Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ASFCYangaSimbaSingidaAzam

Ikiwa imetimia siku zaidi ya 35 tokea msimu wa Ligi kuu kuisha, na siku 20 kabla msimu mpya wa Ligi kuu ya soka Tanzania bara kuanza,vilabu  vyote vipo katika mchakato wa kusajili na kuboresha mabenchi yao ya ufundi.

Swali linakuja, Je kuelekea msimu mpya 2023/24, unaona ni timu gani inaenda kuleta mapinduzi ya kutwaa Ligi kuu au makombe yote?

Katika msimu 2022/ 23 Yanga waliweza kufanya vizuri na kuweza kubeba makombe yote manne ikiwemo Ngao ya jamii, Ligi kuu bara,Azam sports federation na Zanzibar football federation, lakini pia katika Anga la kimataifa Yanga walifanikiwa kushika nafasi ya pili kwenye kombe la shirikisho Afrika.

Kwa maboresho aliyofanya Yanga African ya kupunguza na kuongeza wachezaji na benchi la ufundi,je! ataweza kutetea makombe yake? Inaeleweka Fiston Mayele ameuzwa kwenda pyramids ya Misri, Ikumbukwe Mayele ameondoka Yanga akiwa na rekodi ya kuwa mfungaji bora Ligi kuu bara, akiwa na magoli 17, na pia alifanikiwa kuchukua taji la mfungaji bora kwenye kombe la shirikisho Afrika.

Aliyekuwa mshindi pili ambae ni Simba Sports Club ataweza kufanya mapinduzi ya kuchukua kombe la Ligi au makombe yote, imekuwepo tetesi kuwa Simba ipo katika hatua za mwisho za kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka timu ya Rayon sports ya Rwanda,Leandre Essomba ambae anaongoza Ligi kuu ya Rwanda kwa kuwa na magoli 16.Bila kusahau mzawa wa kazi ngumu ndani ya Simba Mzamiru Yassin,kama ataweza kuvunja rekodi yake kwa msimu wa 2023/24.

kwa upande mwingine, Clatous Chama ataendelea kubaki kwenye nafasi yake kuichezea Simba,baada ya makubaliano yaliyofanyika ya kumuongezea maslahi,kwa safu hii kuna uwezekano wa Simba kufanya vizuri na kurudi kwenye chati yake kama zamani? ikumbukwe Simba sports club imeshika nafasi ya pili katika michuano ya Ligi kuu bara.

Simba SCHuku Azam ikishika nafasi ya tatu, usajili wao umeonekana kuwa tishio kwa mabadiliko ya benchi la ufundi na wachezaji, ikiwa ni Pamoja na aliyekuwa kiungo mchezaji wa Yanga Africans, Feisal Salum (Fei toto) kujiunga na timu ya Azam baada ya kusaini mkataba wa miaka 3. Je! kuna uwezekano wa Azam kukaa nafasi ya kwanza kwa kutwaa kombe la Ligi, na kubeba makombe mengine, ikiwa na kufanya vizuri kwenye michuano ya shirikisho barani Afrika?

Azam FV Ligi KuuKwa upande wa Singida Fountain Gate, imeonekana kuongeza nguvu haswa katika upande wa kubadilisha jina,Pamoja na kuongeza wadhamini wake kwa mabadiliko haya Singida Fountain Gate wataweza kuingia katika kinyang’anyiro cha kuweza kuchukua kombe la Ligi kuu na kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya shirikisho barani Afrika?

Singida FC Tanzania
Bila kusahau kwa upande wa Namungo, kwa msimu uliopita imekosa nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa kwa ngazi ya klabu, ni baada ya kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi kuu bara. je kwa msimu unaokuja Namungo wataweza kufanya mapinduzi kwenye soka la bara? Ikiwa hadi sasa haijafahamika kama kuna usajili wowote umefanyika wa wachezaji wapya na benchi la ufundi.

Kagera Sugar ni moja kati ya timu ambayo inaleta ushindani mkubwa kwenye Ligi kuu, msimu uliopita ilifanikiwa kumaliza kwenye nafasi ya 11, baada ya kupishana pointi nne na Mbeya city iliyoshuka, ikifuatiwa na Polisi Tanzania na Ruvu shooting.

Imekuwepo tetesi za kufanyika usajili wa wachezaji wapya wa kagera sugar hasa kwa upande wa washambuliaji na mabeki, ni kutokana na hali ya timu ilivyokuwa msimu uliopita.

Ni wazi kuwa msimu ujao wa 2023/24 kutakuwa na ushindani mkubwa baina ya timu hizi, ikiwa kila timu imedhamiria kuchukua ubingwa wa Ligi kuu bara, bila kusahau makombe mengine ikiwemo Ngao ya jamii, Azam sports Federation na kombe la shirikisho Afrika.

Mashabiki ni muda wa kuwa tayari kwa ajili ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi Agosti, na Kuendelea pale ambapo mliishia msimu uliopita katika kushangilia timu zenu na kujiandaa kwani lolote linaweza kutokea baina ya timu hizi katika soka la Tanzania.

 

 

 

Share this: