- Vita ya usajili wa dirisha dogo kwenye Ligi Kuu ya NBC 2025/26 imeendelea kutikisa.
- Tayari timu zimetangaza nyota wapya kujiunga na vikosi vyao, huku wengine wakiendelea kujipanga kutambulisha vyuma vipya.
- Kati ya majina ambayo yameshika vichwa vya habari kwa sasa ni Sakata la kiungo Mzambia, Clatous Chama kurejea kwenye kikosi cha Simba.
- Makala hii inakuletea uhalisia wa Tetesi za usajili mpya ndani ya NBC.
Vita ya usajili wa dirisha dogo kwenye Ligi Kuu ya NBC 2025/26 imeendelea kutikisa. Tayari timu zimetangaza nyota wapya kujiunga na vikosi vyao, huku wengine wakiendelea kujipanga kutambulisha vyuma vipya. Kati ya majina ambayo yameshika vichwa vya Habari ni Sakata la kiungo Mzambia, Clatous Chama kurejea kwenye kikosi cha Simba. Makala hii inakuletea uhalisia wa Tetesi za usajili mpya ndani ya NBC.
SOMA HII PIA: Depu straika mpya Yanga, Gueye huyoo Simba: Tetesi usajili mpya Ligi Kuu Bara 2025/26
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Kuhusu Tetesi za usajili wa Chama kurudi Simba

Kwa mujibu wa mchambuzi, Hans Raphael tayari Clatous Chama amesaini mkataba wa mwaka mmoja kurejea Simba SC. Chama anajiunga na Simba SC, akitokea ndani ya kikosi cha Singida Black Stars. Inaelezwa chanzo kikuu ni familia ya staa huyo, ambayo inatamani kuona akirejea Msimbazi.
Hans ameendelea kueleza kuwa viongozi wa Simba wamecharuka, na wanataka kuisuka upya timu hiyo. Taarifa zinasema nusu ya timu inavunjwa, wachezaji wengi wa kigeni wanakatwa na kulete wapya. Mpaka sasa mipango iliyopo ni kuongeza viungo wengine wawili na mshambuliaji.
SOMA HII ZAIDI: Clatous Chama kumalizana na Simba SC sababu zatajwa/ Awesu katambulishwa Police FC Kenya
Waliokamilisha usajili Simba SC kwenye dirisha dogo mpaka sasa

Mpaka sasa Simba SC wamekamilisha usajili na kuwatangaza baadhi ya nyota wakiwemo; Libasse Gueye ambaye inaelezwa amesaini mkataba wa miaka mitatu na Simba. Mnyama pia amewatambulisha walinzi, Nickson Kibabage kutoka Singida Blacj Stars na beki wa kati wa zamani wa Stellenbosch, Osmail Olivier Touré (28). Toure amesaini mkataba wa miaka mitatu. Pamoja na, Simba SC pia imemtambulisha kipa wao mpya Djibrilla Kassali.
Nyota wanaotajwa kuondoka Simba SC

Kiungo, Jean Charles Ahoua (23), Simba SC amemuzwa kwenda Uarabuni na tayari uongozi wa Simba SC, upo kwenye mchakato wa kusaka mbadala. Pamoja na kuendelea kukiwasha Simba, inaelezwa baadhi ya wachezaji huenda wakaachwa wakiwemo, Steven Mukwala na Joshua Mutale.
Mpaka sasa Simba na Mutale wamekubaliana kuachana, Simba SC wanataka kumtoa Mutale kwenda Polisi Kenya Police kwa mkopo. Tayari Simba SC na Polisi Kenya wamekubaliana kila kitu, ila Changamoto viongozi wa Simba SC hawajakutana na Budo. Nyota huyo amejibu kuwa yuko tayari kuondoka Simba SC, ila siyo kwa mkopo bali Simba SC wavunje mkataba wake uliobaki kisha wamlipe hela yake aondoke. Ikumbukwe Budo amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
SOMA HII ZAIDI: Feisal Salum ‘Feitoto’ ashtua! tetesi za usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26
Hitimisho
Kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo ni nyakati muhimu ya maboresho ya vikosi kwa ajili ya nusu ya pili ya msimu. Ni wazi mashabiki na viongozi wanaposhabikia tetesi za usajili mpya wanapaswa pia kuzingatia ubora wa wachezaji ambao wanasajiliwa kwa kuwa usajili huu unahitaji nyota walio kwenye ubora na sio wa majaribio. Kila la kheri kwa nusu ya pili ya msimu.

