- Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2025), yamemalizika kwa Bingwa Senegal kuwafunga Morocco 1-0.
- Ukiachana na stori za kupokonyana mataulo ya makipa na Senegal kugomea mchezo.
- Stori kubwa kwa sasa ni kurejea kwa mashindano ya ndani na ya Afrika.
- Katika CAFCL, Al Ahly vs Young Africans SC ni mchezo unaotazamwa na kusubiriwa na wengi.
Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2025), yamemalizika kwa Bingwa Senegal kuwafunga Morocco 1-0. Achana na stori za kupokonyana mataulo ya makipa na Senegal kugomea mchezo. Stori kubwa kwa sasa ni kurejea kwa mashindano ya ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika CAFCL, Al Ahly vs Young Africans SC itavaana na Al Ahly ya Misri siku ya Ijumaa, Makala hii inakupa dondoo muhimu kuelekea ratiba hiyo.
SOMA HII PIA: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC) 2025/26, kimataifa ni Al Ahly vs Yanga SC
Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.
Al Ahly vs Young Africans, Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Yanga wanatarajiwa kuwa na michezo miwili migumu, itakayofuatana dhidi ya Al Ahly. Mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa nchini Misri Ijumaa ya Januari 23, mwaka huu na mchezo wa marudiano ukipigwa Januari 30, mwaka huu. Ikumbukwe michezo hii ni mwendelezo wa mechi za hatua ya Makundi ya Caf Champions League. Ikumbukwe kwenye mashindano hayo ni Yanga SC NA Simba SC zinaiwakilisha Tanzania.
Al Ahly SC vs Yanga SC, Wananchi haoo wanawafuata Waarabu Misri
Kuelekea ratiba ya mechi hizo, uongozi wa Yanga SC umethibitisha kuwa kikosi chao kinatarajiwa kuondoka usiku huu Kwenda Misri. Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa, wanatarajia kutoa majina ya wachezaji watakaosafiri. Hilo litafanyika mara tu, safari itakapoanza.
Diarra aongeza mzuka

Kama sehemu ya kukiongezea nguvu kikosi cha timu hiyo, hatimaye mlinda mlango namba 1 Djigui Diarra amewasili Tanzania. Nyota huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Mali, ambacho kilikuwa kikishiriki AFCON 2025 nchini Morocco. Diarra alikuwa nyota muhimu ambaye aliisaidia Mali kucheza hatua ya Robo Fainali kabla ya kuondoshwa na Senegal.
SOMA HII ZAIDI: Ratiba ya mechi za CAF Champions League 2025/26/ Matokeo na magoli
Yanga SC yapasha kiporo kwa kishindo

Yanga SC wanauendea mchezo dhidi ya Al Ahly wakiwa na ari kubwa, mara baada ya kuibuka na ushindi mzito wa mabao 6-0 dhidi ya Mashujaa. Mchezo huo ulipigwa Jumatatu kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge Dar es Salaam.
Ratiba ya viporo vingine vya ligi Kuu Bara NBC vilivyochezwa;
Dodoma Jiji vs Singida Black Stars
Azam FC vs Coastal Union
Simba SC vs Mtibwa Sugar
Huku Yanga SC wakirejea kwa kasi, watani zao wa jadi Simba SC wao walishuka dimba la Meja Jenerali Isamuhyo kuikaribisha Mtibwa Sugar. Simba walikubali kuangusha pointi 2 kutokana na sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kwa Kocha wao mpya, Steve Barker.
Ikumbukwe Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), ilitangaza rasmi msimu huu mpya wa 2025/26 kuanza rasmi Septemba 17, 2025 mwaka huu na inatarajiwa kuisha Mei 30, mwaka 2026. Bingwa mtetezi wa ligi hiyo inayodhaminiwa na NBC ni klabu ya Yanga SC. Wananchi wanafurahia msuli wa kifedha, kutoka kwa mdhamini wao mkuu 17 Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.
SOMA HII PIA: CAF Champions League matokeo mechi zote hatua ya makundi 2025/26
Hitimisho

Al Ahly vs Young Africans SC unatarajiwa kuwa zaidi ya mchezo, hii ni vita ya thamani ya kuisaka Robo Fainali. Kila timu itajaribu kuboresha takwimu za kukutana kwao, ambapo mpaka sasa Al Ahly amekuwa bora. Katika michezo 8 waliyokutana waarabu wameshinda mechi 5, Yanga wameshinda mechi moja tu, huku mechi 2 zikimalizika kwa sare.

