Musonda ZambiaMusonda Zambia
  • Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), yanaendelea kutimua vumbi nchini Morocco.
  • Mashindano hayo kwa sasa yameingia hatua ya mtoano ya timu 16 bora.
  • Katika kuingia hatua hiyo, tayari baadhi ya timu zimeyaaga mashindano.
  • Makala hii inakuletea nchi 5 ambazo zimeaga mashindano mapema.                                   

Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), yanaendelea kutimua vumbi nchini Morocco. Mashindano hayo kwa sasa yameingia hatua ya mtoano ya timu 16 bora. Katika kuingia hatua hiyo, tayari baadhi ya timu zimeyaaga mashindano. Makala hii inakuletea nchi 5 ambazo zimeaga mashindano mapema.     

SOMA HII PIA: AFCON 2025 hatua ya makundi matokeo na ratiba/ Msimamo, tarehe

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

AFCON 2025: Nchi hizi 5 zimeaga mashindano mapema

Gabon
Gabon

Takriban nchi tano zimeondolewa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025, AFCON nchini Morocco.

Katika Matchday 2 Zimbabwe ndiyo timu ya mwisho kutoka Kundi B, Nchi hiyo imeondoshwa katika michuano hiyo kufuatia kukamilika kwa mechi za mwisho za Kundi B. Zimbabwe iliaga mashindano jana Jumatatu.

Ikumbukwe Zimbabwe ilifungwa mabao 3-2 na Afrika Kusini na kumaliza mkiani mwa kundi hilo ikiwa na pointi moja.

Kwa matokeo hayo, Zimbabwe imeungana na Botswana, Gabon, Equatorial Guinea na Zambia, ambayo ilichapwa mabao 3-0 na Morocco katika mchezo wa Kundi A, kufuzu michuano hiyo.

SOMA HII ZAIDI: AFCON 2025 Mahrez, Jackson, Achouri watikisa: Hawa hapa wafungaji bora wa Raundi ya 1

Timu hizi 3 zashindwa kuvuna pointi ndani ya dk 180

Dube rekodi
Dube rekodi

Botswana, Equatorial Guinea na Gabon zilitolewa baada ya kukamilika kwa awamu ya pili ya mechi za makundi. Nchi hizo tatu zilishindwa kupata pointi hata moja katika mechi zao mbili za ufunguzi.

Hitimisho

AFCON 2025 inaendelea kutifuana huko Morocco. Ujazo wa uwezo ulionao ndio utakufanya usalie kwenye mashindano. Mapema tu, wale ambao uwezo wao umekuwa na mashaka wameaga mashindano na kwa kuwa mashindano yanaendelea tunatarajia timu zaidi kutolewa. Kila mmoja anatamani kuona ni timu zipi zitafika hatua ya 16 bora.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.