- Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itaanza punde tu, baada ya kukamilika kwa ratiba ya mechi za kimataifa.
- Yanga SC vs AS FAR CAF mchezo utakaopigwa Novemba 22, 2025 umeanza kuwa gumzo.
- Hii ni kutokana na ubora na utajiri mkubwa, wa historia kwa timu hizi katika mashindano ya kimataifa.
Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika inatarajia kuanza punde tu, baada ya kukamilika kwa ratiba ya mechi za kimataifa. Yanga SC vs AS FAR CAF mchezo ambao utapigwa siku ya tarehe 22 Novemba 2025, umeanza kuwa gumzo. Hii ni kutokana na ubora na utajiri mkubwa, wa historia kwa timu hizi katika mashindano ya kimataifa. Uongozi wa kikosi cha Yanga SC chini ya kocha mkuu mpya, Pedro Goncalves umejichimbia kuwaandalia waarabu dozi.
SOMA HII PIA: Makundi Klabu Bingwa Afrika CAF 2025/26 haya hapa | Simba SC na Yanga SC zapewa waarabu
Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Je, bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Yanga wamepangwa dhidi ya timu gani makundi

Katika droo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/26, ambayo yalipangwa nchini Afrika Kusini Novemba 3, mwaka huu. Yanga SC wamefanikiwa kupangwa kwenye Kundi B pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, AS FAR ya Morocco na JS Kabylie ya Algeria. Makundi mengine ni kama ifuatavyo:
Kundi A
RS Berkane kutoka Morocco
Pyramids FC kutoka Misri
Rivers United kutoka Nigeria
Power Dynamos kutoka Zambia
Kundi C
Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini
Al Hilal kutoka Sudan
MC Alger kutoka Algeria
St Eloi Lupopo ya Congo
Kundi D
ES Tunis ya Tunisia
Simba SC kutoka Tanzania
Petro Luanda ya Angola
Stade Malien ya Mali
SOMA HII ZAIDI: Tanzania NBC Premier League table & standings 2025-26 season
Hatua ya makundi itaanza kutimua vumbi lini?

Hatua ya makundi ya CAF Champions League yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21,2025, kwa michezo yam kondo wa kwanza. Hatua hii itaendelea mpaka kila timu itakapomaliza mechi zake 6, yaani 3 za ugenini na 3 za nyumbani. Kutoka kwenye kila kundi zinatafutwa timu mbili, ambazo zitasonga hatua ya robo fainali.
Safari ya Yanga SC mpaka kufika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika?

Yanga SC kutoka Tanzania ilianzia katika hatua ya awali. Katika hatua hiyo walicheza mechi nne, mbili ugenini na mbili ikiwa nyumbani. Hatua ya kwanza ilianza dhidi ya Wiliette SC kutoka nchini Angola na kufanikiwa kupata ushindi wa jumla wa magoli 5-0.
Hatua ya pili ya awali Yanga SC iliyokuwa inanolewa na kocha Romain Folz ilivaana na Silver Striker ya Malawi. Ugenini ilipoteza kwa kufungwa goli 1-0, katika mchezo ulioondoka na kibarua cha Folz. Kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Yanga SC ilifanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0 na ikasonga mbele kutinga hatua ya makundi.
SOMA HII PIA: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 NBC Premier League, CAF Champions League/ Live scores
Yanga SC kuisaka Robo Fainali Zanzibar
Uongozi wa Yanga SC kupitia kwa Ofisa Habari wake, Ali Kamwe umeutangazia Umma wa soka na mashabiki wake kuwa mechi zao zote tatu za kimataifa hatua ya makundi zitapigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Huu ndio unatarajia kuwa uwanja wao wa nyumbani. Yanga SC vs AS FAR ndiyo karata ya kwanza kwa Yanga Novemba 22, mwaka huu.
Ratiba kamili ya Yanga SC hatua ya makundi CAF Champions League
Yanga SC vs AS FAR inatarajiwa kuchezwa Novemba 22, 2025
JS Kabylie vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa Novemba 28, 2025
Al Ahly vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa Januari 23, 2026
Yanga SC vs Al Ahly inatarajiwa kuchezwa Januari 30, 2026.
AS FAR vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa 6, Februari 2026.
Yanga SC vs JS Kabylie inatarajiwa kuchezwa Februari 13,2026.
Yanga SC vs AS FAR, Kocha Pedro awaandalia Waarabu dozi

Kwa kutambua uzito wa timu ambazo wanatarajia kuvaana nazo na mchezo dhidi ya AS FAR, kocha mkuu wa Yanga, Pedro ameendelea kuwapa mazoezi mazito mastaa wake waliosalia kambini. Katika ripoti mbalimbali ambazo zimetolewa na uongozi wa timu hiyo,zinaonyesha mazoezi makali yakiendelea Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.
Hitimisho
Kuelekea mchezo wa Yanga SC vs AS FAR CAF, Licha ya ubora wa AS FAR ambao wanauonyesha katika ligi ya Morocco wakishika nafasi ya pili. Bado umadhubuti wa Yanga SC kwenye mashindano ya kimataifa umezidi kuimarika. Misimu miwili iliyopita walicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mashabiki wao wanatamani kuona timu inaandika rekodi nyingine kubwa zaidi msimu huu, hasa baada ya kuishia makundi msimu uliopita.

