- Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League Oktoba 25,2025 Uwanja wa Mkapa ni mchezo wa maamuzi ya timu itakayotinga hatua ya makundi.
- Clement Mzize kuna hatihati kukosekana kwa mara nyingine katika mchezo wa CAF.
- Silvers Strikers 1-0 Yanga SC mchezo wa mwisho kwa Romain Folz kukaa kwenye benchi la ufundi, Malawi.
Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League Oktoba 25,2025 utakuwa mchezo wa kwanza bila ya Romain Folz, Uwanja wa Mkapa. Hii ni baada ya Folz kufutwa kazi Oktoba 18, 2025 muda mchache baada ya kupoteza Uwanja wa Bingu matokeo yalikuwa Silver Strikers 1-0 Yanga SC. Goli la Andulu Yosefe dakika ya 76 liliharibu sherehe ya wananchi kwenye mchezo huo. Jumamosi wababe hawa watakuwa uwanjani kwenye mchezo wa marudiano.
SOMA HII: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League 2025| Lineup, H2H
Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League nani kutinga hatua ya makundi?

Hii ni karata muhimu kwa timu zote mbili Uwanja wa Mkapa. Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League Oktoba 25 imeshikilia mshindi wa hatua ijayo. Mtihani mkubwa upo kwa Yanga SC kusawazisha goli la ugenini na kutafuta goli la ushindi. Hivyo ili akate tiketi kutinga hatua ya makundi angalau apate ushindi wa goli 2-0.
Silver Strikers goli la nyumbani linawapa nguvu kutanguliza mguu mmoja kimataifa. Wanahitaji sare ya aina yoyote ili kutinga hatua ya makundi. Ikiwa watafungwa goli 1 mpaka mwisho wa mchezo mshindi atapatikana kwa penati.
Clement Mzize wa Yanga SC kukosekana?
Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League kuna uwezekano mshambuliaji Clement Mzize akakosekana. Mzize alikuwa na maumivu ya goti licha ya kuanza mazoezi na wachezaji wenzake bado hajawa fiti. Hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza mchezo uliopita ugenini.
Meneja Yanga SC Walter Harson maoni yake
Walter Harson, Meneja wa Yanga SC ameweka wazi wataandika historia Jumamosi. Licha ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Silvers Strikers bado anaamini wanakwenda kufanya jambo kubwa. Aliongeza kuwa matokeo yatatafutwa Uwanja wa Mkapa.
“Hii ni Champions League kuna mechi mbili za kucheza. Tunakwenda kuandika historia kwenye mchezo wa Jumamosi Uwanja wa Mkapa. Tunaamini kwamba tutafanya vizuri na kutinga hatua ya makundi.
“Mashabiki watambue kwamba matokeo ya mchezo uliopita hayo yamekwisha hivyo kwa sasa tunafanya maandalizi kwa mchezo wetu ujao, Timu ipo vizuri na wachezaji wanahitaji kuona tunapata ushindi,”.
SOMA HII: Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League | H2H, takwimu muhimu, utabiri

Mechi 7 za Yanga SC zilizopita

Septemba 12,2025 – Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki).
Septemba 16, 2025 – Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).
Septemba 19, 2025 – Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika
Septemba 24,2025 – Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).
Oktoba 27,2025 -Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Septemba 30,2025, Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).
Silver Strikers FC 1-0 Yanga SC , Oktoba 18, 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi 7 za Silver Strikers zilizopita

Silver Strikers 1-0 Chitipa United, mchezo wa League Agosti 27 2025.
Shire FC 1-4 Silver Strikers, Septemba 11 2025 Malawi Cup
Elgeco Plus 1-1 Silver Strikers, Septemba 21 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Silver Strikers 0-0 Elgeco Plus Septemba 27 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Blue Eagles 0-3 Silver Strikers Oktoba 2 2025, Malawi Cup.
Bullets 2-1 Silver Strikers Oktoba 5 2025, Malawi Cup.
Silver Strikers FC 1-0 Yanga SC, Oktoba 18, 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.
SOMA HII: Yanga SC 0-1 Silver Strikers CAF Champions League 2025 | Highlights, goal

H2H
Silver Strikers FC 1-0 Yanga SC CAF Champions League, Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu, Malawi.
Yanga SC vs Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025.
Hitimisho
Yanga SC vs Silver Strikers CAF Champions League utakuwa mchezo wa kwanza kwa kocha msaidizi Patrick Mabedi kuongoza bila Folz. Silvers Strikers wanawinda rekodi kutinga hatua ya makundi je wananchi watashinda mtego huo? Hapa tutaendelea kukupa taarifa muhimu za mchezo site ya SportPesa.
Una nafasi kubwa leo kushinda mamilioni na Supa Jackpot 17, bofya hapa


