- Mfalme wa nyika ameunguruma huko katika ardhi ya Eswatini.
- Hii ni baada ya ubao wa Uwanja wa Somhlolo kuonyesha Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC baada ya dakika 90.
- Kibu Denis aibuka shujaa baada ya kufunga mabao 2 dakika za mwisho.
Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, ndivyo ubao wa matokeo umesomeka mara baada ya dakika 90 huko Eswatini. Matokeo hayo ni ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya pili ya awali. Mchezo huu umepigwa leo Oktoba 19, 2025 Uwanja wa taifa wa Somhlolo.
Shinda sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Hizi hapa ‘Highlights’ za mechi ya Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Somhlolo, nchini Eswatini ulikuwa na ushindani mkubwa. Kipindi cha kwanza timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu, huku Simba SC wakifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi. Bao la kwanza la mchezo huo lilikuja dakika ya 45 ya mchezo, kupitia kwa mlinzio wa Simba SC, Wilson Nangu.
Nangu alifunga bao hilo la kuongoza kwa kuunganisha kwa kichwa krosi nzuri ya kona ya kiungo, Neo Maema. Mara tu, baada ya bao hilo kipyenga cha mwamuzi kikasikika na timu Kwenda mapumziko. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa, huku kila timu ikisaka bao.
Mara baada ya majaribio kadhaa Simba SC walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa, Kibu Dennis dakika ya 82. Kibu alifunga bao hilo akitumia pasi ya kisigino ya Jonathan Sowah. Dakika 8 baadaye, Kibu aliiandikia tena simba bao la 3 ambalo kwake lilikuwa bao la 2 kwenye mchezo.
SOMA HII ZAIDI: Nsingizini Hotspurs vs Simba SC CAF Champions League| Mtihani wa kwanza wa Meneja Mkuu Pantev
Kibu Denis ‘Super Sub’

Nyota wa Simba SC, Kibu Denis ameifungia timu hiyo mabao mawili muhimu lakini nyota huyo alifanya hayo yote akitokea benchi. Kibu aliingia dakika ya 66 akichukua nafasi ya Jean Charles Ahoua. Ikumbukwe bao lake la pili alifungwa dakika ya 90, akitumia nafasi iliyotengenezwa na Morice Abraham.
Mlinzi Wilson Nangu aliyeifungia Simba SC bao la kwanza alishindwa kukamilisha dakika 90, hii ni baada ya kupata maumivu na nafasi yake kuchukuliwa na mlinzi Karabou Chamou.
Kikosi cha Simba SC kilichoanza
Kipa: Yakoub Suleman
Mabeki: Anthon Mligo, Shomari Kapombe, De Reuck na Wilson Nangu
Viungo: Joshua Mutale, Jean Ahoua, Naby Camara, Ellie Mpanzu na Neo Maema
Mshambuliaji: Seleman Mwalimu
Wachezaji wa akiba: Hussen Abel, David Kameta, Chamou, Yusuph Kagoma, Ladack Chasambi, Jonathan Sowah, Steven Mukwala, Morice Abraham na Kibu Dennis.
Orodha ya wachezaji wote wa Simba SC waliosafiri mpaka Eswatini ni:
Makipa: Yakoub Suleiman, Hussen Abel
Mabeki: Shomari Kapombe, David Kameta, Anthony Mligo, Karabou Chamou, Rushine De Reuck, Wilson Nangu, Vedastus Masinde
Viungo:
Yusuph Kagoma, Mzamiru Yassin, Naby Camara, Joshua Mutale, Kibu Dennis, Elie Mpanzu, Ladack Chasambi, Jean Ahoua, Neo Maema, Morice Abraham
Washambuliaji: Jonathan Sowah, Steven Mukwala na Seleman Mwalimu.
Mastaa wa Simba SC walioshindwa kusafiri

Moussa Camara, kipa namba moja wa Simba SC anaendelea kukosekana kutokana na majeraha. Wengine ni mlinzi, Hamza Jr Pamoja na viungo, Mohamed Bajaber na Allasane Kante. Baadhi ya mastaa hao wanakosekana kutokana na kutokuwa fiti.
SOMA HII ZAIDI: Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League | H2H, statistics, lineups
Ushindi wa kwanza kwa Meneja Dimitar Pantev

Ushindi huu sio muhimu tu, kwa Simba SC bali pia kwa bosi wao mpya wa benchi la ufundi meneja mkuu Pantev. Raia huyu wa Bulgaria amekuja kuchukua majukumu yaliyoachwa na kocha, Fadlu Davis aliyetimkia Raja Casablanca. Pantev amejiunga na Simba SC, akitokea ndani ya kikosi cha Gaborone United.
Simba ilipata mafanikio makubwa na ya haraka chini ya kocha Fadlu, na huu umebaki kuwa mtihani mwingine kwa Pantev ambaye ameanza vizuri safari yake ndani ya Simba SC. Mabosi wa Simba SC walilazimika kuilipa fidia Gaborone United, ili kumpata meneja huyo. Hii ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya kufanikisha uhamisho kwa kuwa bado alikuwa na mkataba.
SOMA HII PIA: Nsingizini Hotspurs vs Simba SC CAF Champions League| Mtihani wa kwanza wa Meneja Mkuu Pantev
Hitimisho
Mechi ya mkondo wa kwanza yaNsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC inawaweka wawakilishi hao kutokea Tanzania, katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya makundi. Hii itaifanya timu hiyo ambayo ipo nafasi ya 5 kwa ubora Afrika, kuandika historia mpya ya kucheza hatua ya makundi ‘back-to-back’. Bado mechi haijaisha na Simba wana kazi kubwa ya kufanya Oktoba 26, kwenye mchezo wa marudiano.

