Simba SC vs Gor Mahia FCFadlu Davids Head
  • Wachezaji watatu Simba SC wameanza kwa majanga kutokana na kuondolewa kwenye mpango katika mchezo wa kwanza wa ushindani.
  • Kuelekea Kariakoo Dabi Yanga SC vs Simba SC tambo zatawala kwa makocha wa timu zote na manahodha kila mmoja akivutia kwake.
  • Ahmed Arajiga mwenye beji ya FIFA ametangazwa kuwa mwamuzi wa kati katika mchezo huo wenye presha kubwa nje na ndani ya uwanja Septemba 16 2025.

Kuelekea Kariakoo Dabi Yanga SC vs Simba SC tambo zatawala. Makocha na manahodha wamebainisha kuwa wapo tayari kwa fainali ya Ngao ya Jamii. Sio Yanga SC wala Simba SC wote wametunishiana misuli kulitaka taji. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 16 2025, Uwanja wa Mkapa.

Muda wa kuvuna mamilioni ukipaisha Kindege cha SportPesa

Rubani kicheko kinakusubiri ukipaisha Kindege cha SportPesa. Mamilioni yapo kwenye mgao kwa ajili yako. Rahisi, cheza Aviator upate mgao wako sasa hivi.

image

Kuelekea Kariakoo Dabi Yanga SC vs Simba SC sikia tambo za Romain Folz kocha wa Yanga SC

Kuelekea Kariakoo Dabi Yanga SC vs Simba SC
Folz Kocha Mkuu wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Soma hii: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2025/26

Kuelekea Kariakoo Dabi Yanga SC vs Simba SC tambo za makocha zimetawala. Huyu hapa ni Romain Folz Kocha Mkuu wa Yanga SC anasema: “Msimu umeanza tunayo shauku kubwa ya matokeo mazuri. Tunakwenda kucheza mchezo mkubwa, lazima tuhakikishe mashabiki wanapata kile ambacho wanahitaji.

“Mtarajie kuiona Yanga SC tofauti katika upangwaji wa kikosi chetu na hata kiuchezaji. Tumecheza michezo mingi ya kirafiki tumeshinda na tulicheza vizuri pia lakini mchezo wa kesho ni mchezo wa ubingwa hivyo ni muhimu kupata matokeo.

“Tunakwenda kwenye mchezo mkubwa, tunapaswa kuwaheshimu wapinzani na tumejiandaa kukabiliana na kila hali ya mchezo. Nina kundi kubwa la wachezaji wazuri ambao wanaweza kumudu mazingira ya mchezo wowote, tumejiandaa vizuri kimwili na kiakili. Sina majeruhi wapya na kikosi changu kipo imara kutafuta ubingwa.

Nahodha wa Yanga SC, Dickson Job

Job Kapten
Job Dickson beki wa Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Soma hii: Uchambuzi wa Yanga SC vs Simba SC itakayochezwa Septemba 16 | H2H, vikosi, matokeo, wafungaji – SportPesa Tanzania

“Tunajua mechi yetu ya Derby ni mechi ngumu, licha ya ugumu huo sisi tuna timu imara ambayo inaweza kupata matokeo katika mazingira magumu, lazima tupambane tuendelee kulinda heshima ya timu yetu.

“Kila mchezaji anapaswa kujua kesho ni muhimu mno kupambana ni mchezo muhimu sana kwetu kwani inaonesha dalili nzuri kuelekea msimu mpya. Tupo tayari na mashabiki wajitokeze kwa wingi,”.

Huyu hapa Kocha Mkuu wa Simba SC Fadlu Davids

Kocha mkuu wa Simba Fadlu Davids amebainisha kuwa hawana presha kubwa zaidi kuliko ile iliyopo kwa wapinzani wao Yanga SC. Fadlu amebainisha sababu muhimu huku akiweka wazi kuwa wapo tayari kupambana. Aliongeza kuwa makosa waliyofanya wakati ule yamefanyiwa kazi.

“Presha kubwa itakuwa kwa upande wa Yanga SC kwa kuwa wanabenchi jipya la ufundi. Lakini wametoka kupata matokeo katika michezo mingi dhidi yetu. Hivyo naamini watakuwa na presha kubwa ya matokeo kuliko sisi.

“Najua tumepoteza Dabi zilizopita naamini katika mchezo wa kesho tunatakiwa kupata matokeo. Tupo tayari kwaajili ya mchezo na naamini wachezaji wanatambua umuhimu wa kushinda mchezo huu muhimu.”

 Shomari Kapombe nahodha wa Simba SC

Shomari Kapombe nahodha wa Simba SC alibainisha kuwa kuna uimara kwa wapinzani Yanga SC sehemu ya ushambuliaji. Jambo hilo linawafanya wawe makini. Aliongeza kuwa makosa wamefanyia kazi kuwa imara.

“Tunafahamu kuwa Yanga SC wanasafu nzuri ya ushambuliaji na msimu uliopita walifunga mabao mengi. Tayari tumepokea maelekezo mengi kutoka kwa mwalimu jinsi ya kuwakabili washambuliaji wa Yanga SC.

“Tunafahamu tumepoteza michezo mingi iliyopita, mchezo huu ni mchezo wa kufungua msimu na ni mchezo wa ubingwa hivyo tumejipanga kupata matokeo mazuri ili tuweze kuwapa furaha mashabiki wetu. Tupo tayari.”

Waamuzi wa Kariakoo Dabi hawa hapa

Ahmed Arajiga
Ahmed Arajiga mwamuzi mchezo wa Kariakoo Dabi Septemba 16 2025.

Soma hii: Kariakoo Dabi kuna vita nyingine kwa wachezaji

Mwamuzi wa kati ni Ahmed Arajiga,  mwamuzi msaidizi ni Mohamed Mkono, mwamuzi msaidizi namba 2 ni Kassim Mpanga, mwamuzi wa akiba ni Ramadhani Kayoko na mtathimini waamuzi ni Soud Abdi.

Wachezaji watakaokosekana

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Romain Folz alibainisha kuwa wapo wachezaji watakaokosekana dhidi ya Simba SC. Kocha huyo hakuwa tayari kuwataja majina.Taarifa zinaeleza kuwa Pacome Zouzoua ambaye alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania mazoezi ya mwisho yataamua hatma yake.

Bajaber Kambini
Bajaber miongoni mwa nyota wa Simba SC watakaoikosa Kariakoo Dabi. Source: Simba SC.

Soma hii: Kariakoo Dabi vita ya Diarra na Camara inaanza | Takwimu, mechi, magoli | Septemba 16 2025 – SportPesa Tanzania

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids amewataja wachezaji watatu ambao watakosekana. Miongoni mwa wachezaji hao ni Allassane Kante, Mohamed Semfuko na Mohamed Bajaber. Wachezaji hawa walipata maumivu kwenye maandalizi ya msimu mpya 2025/26 nchini Misri.

Licha ya kuwakosa wachezaji hao Fadlu alibainisha kwamba wapo tayari kwa mchezo. Aliongeza kuwa walikuwa na muda mzuri wa maandalizi jambo linalowapa nguvu kufanya vizuri. Alibainisha kwamba mashabiki wajitokeze kwa wingi.

Hitimisho

Kuelekea katika Kariakoo Dabi Yanga SC imekuwa na matokeo mazuri mbele ya Simba SC. Katika mechi tatu za msimu wa 2024/25 zote ilipata ushindi. Ndani ya dakika 270 safu ya ushambuliaji ya Yanga SC ilifunga magoli manne na ile ya Simba SC haikufunga.

image
Share this: