Balla ConteBalla Conte
  • Orodha ya wachezaji waliosajiliwa na Yanga SC 2025/26 na wale waliongezewa mikataba inazidi kuongezeka.
  • Vita yao kwenye kunasa saini za wachezaji wapya na Simba SC inaogopesha, misuli wanatunishiana sokoni.
  • Ali Kamwe abainisha ujanja wa Yanga SC ulipo, Ahmed Ally wa Simba SC aishia kukubali uwezo wa Conte.

Kuna Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Yanga SC 2025/26 kueleka msimu mpya ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Usajili wa Yanga SC ni balaa zito wakishinda wakionekana kushinda vita mbele ya watani zao wa jadi Simba SC katika kuwania saini za wachezaji. Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC alibainisha kuwa watamsajili mchezaji yeyote wanayemtaka.

Msikie Ali Kamwe wa Yanga SC

Yanga kupeleka Kombe la ubingwa wa ligi ya NBC Ikulu
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC imekomalia saini ya Balla Conte

Shinda mamilioni ukipaisha kindege

Ukipaisha kindege sasa hivi unashinda mamilioni ni rahisi kweli. Wikiendi inamalizwa kishujaa kwa kila rubani. Cheza Aviator upate mgao wako sasa.

Aviator banner

“Ambacho ninatambua ni kwamba tupo kwenye kufanyia maboresho timu yetu. Mchezaji yoyote ambaye tutakuwa tunamuhitaji mashabiki wa Yanga SC wakichangia kwenye tofali la ubingwa kazi itakuwa rahisi. Ili kupata mchezaji fedha inahitajika, maandalizi yanahitaji fedha tupo tayari kwa ushindani kuelekea msimu mpya 2025/26,” alisema Kamwe.

Miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakitajwa kwa ukaribu kusajiliwa na Simba SC ni Balla Conte. Yanga SC tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa walikwama kupata saini ya mchezaji huyo baada ya Simba SC kuweka dau kubwa. Mwisho mchezaji alitambulishwa Yanga SC.

Simba SC kuhusu Conte

Med Kicheko
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Simba SC kufanya usajili mkubwa

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC aliwahi kubainisha kuwa Conte ni mchezaji mzuri. Ahmed aliongeza kuwa ikiwa wataipata saini ya kiungo huyo furaha itakuwa kubwa Msimbazi. Hesabu ziligonga mwamba mwishoni.

“Conte ni mchezaji mzuri na anajua mpira. Kwa namna ambavyo tumemuona tukimpata Simba SC itakuwa ni furaha. Wanasimba wakae tayari kwani Conte ni mchezaji anayepaswa kucheza Simba SC,” alisema Ahmed.

Hapa tunakuletea usajili wa Yanga SC uliokamilika. Ikumbukwe kwamba ni kuelekea msimu mpya wa 2025/26. Yanga SC itakuwa chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz. Hawa hapa wachezaji wapya na walioongeza mikataba Yanga SC:-

Ninju

Abubakar Nizar Othuman, maarufu kwa jina la Ninju. Huyu ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC kwa msimu wa 2025/26. Mlinzi huyu amesajiliwa na Yanga SC kutoka Azam FC alitambulishwa rasmi Julai 27 2025.

Lassine Kouma

Kouma
Kouma Lassine ingizo jipya Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Lassine Kouma mrithi wa Khalid Aucho Yanga SC

Lassine Kouma ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC kuelekea msimu wa 2025/26. Kiungo huyo amekabidhiwa rasmi jezi namba 8.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 jezi namba 8 ilikuwa inamtambulisha kiungo Khalid Aucho raia wa Uganda. Kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien. Julai 25 alitambulishwa kuwa mali ya Yanga SC. Alikuwa anatajwa kwenye rada za Simba SC,

Balla Conte

Usajili wake ulikuwa na mvutano mkubwa kutokana na watani zao wa jadi Simba SC kutajwa kuwa kwenye hesabu kuinasa saini yake. Mwisho kiungo huyo alitambulishwa Jangwani. Ni njano na kijani kwa msimu wa 2025/26.

Ni Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia. Nyota huyu mpya alisaini mkataba wa miaka mitatu.

Mudathir Yahya

Mzee was imu ziite uhakika kuwa kwenye uzi wa kijani na njano 2025/26. Tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa Simba SC inahitaji saini yake. Ni kiungo ambaye alikuwa chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi, msimu wa 2024/25.

Mudathir Yahya Julai 22 2025 aliongeza mkataba wa miaka miwili. Atakuwa ndani ya Yanga SC mpaka 2027. Alikuwa kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa ligi inayodhaminiwa na NBC.

Offen Chikola

Offen Chikola
Offen Chikola ingizo jipya Yanga SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Soma hii: Offen Chikola atambulishwa Yanga SC

 Nyota Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo. Mzawa huyu alikuwa anatajwa kwenye rada za Simba SC.

Casemiro

 Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Huyu ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania nafasi ndani ya uwanja.

Dennis Nkane

Kiungo mshambuliaji Dennis Nkane aliongeza mkataba wa miaka miwili mpaka 2027. Nkane hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza msimu wa 2024/25. Kazi kubwa itakuwa kwenye kupambania namba msimu mpya chini ya kocha mpya.

Nkane alitambulishwa rasmi kuongeza mkataba Ilikuwa ni Julai 25 2025. Hivyo bado mchezaji huyo ataendelea kuwa Jangwani. Awali alikuwa anatajwa kuwa huenda asingeongezewa kandarasi mpya.

Pacome

Pacome na Injinia
Pacome na Injinia Hersi Said ambaye ni Rais wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Pacome Zouzoua yupo Yanga SC asaini miaka miwili

Kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua aliongeza mkataba wa miaka miwili Julai 24 2025. Nyota huyu alikamilisha msimu akiwa kafunga jumla ya mabao 12 na pasi 10. Kwenye mabao hayo 12 alifunga mabao mawili kwa penati. Alikuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na Simba SC.

Pacome yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC msimu wa 2025/26. Ni miongoni mwa wachezaji waliovaa medali kwenye mchezo wa fainali Kombe la Shirikisho Afrika. Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia akiwa kafunga mabao 7, ule wa kushoto ni manne na kwa pigo la kichwa bao moja ilikuwa dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Hitimisho

Yanga SC inatajwa kuwa kwenye hatua za mwisho kuwatangaza nyota wake wengine walioongeza kandarasi. Beki Dickson Job ambaye yupo kwenye timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatajwa kaongeza kandarasi ya miaka miwili. Maxi Nzengeli muda wowote naye atatangazwa kuongeza mkataba.

sportpesa jackpot
Share this: