MbappeMbappe
  • PSG vs Real Madrid Julai 9 2025 live moto utawaka kwenye Uwanja wa MetLife.
  • Timu hizi zimekutana mara 11 katika historia, huku Madrid wakionyesha ubabe wa kushinda mara 6, sare 2 na kupoteza mara 3.
  • Mchezo huu unatajwa kuwa mpambano wa wachezaji wanaoshindania Ballon d’Or, kwa mwaka huu Mbappe na Dembélé

Moto utawaka pale Mabingwa wawili wakubwa duniani wanakutana katika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu, katika mechi ya PSG vs Real Madrid Julai 9 2025 live ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa MetLife nchini Marekani, huku kwa majira ya Afrika Mashariki mchezo huo unatarajiwa kupigwa kesho Julai 8, saa 4:00 usiku.

PSG vs Real Madrid Julai 9 2025 live ni vita ya Ballon d’Or

PSG vs Real Madrid
PSG vs Real Madrid

Mchezo huu muhimu unatajwa kuwa ni mpambano wa wachezaji wanaoshindania Ballon d’Or, kwa mwaka huu ambapo Kylian Mbappé na Ousmane Dembélé wanakutana, ingawa kati yao hakuna hata mmoja aliyeanza mechi katika mashindano haya kutokana na majeraha madogo.

Badala yake, vilabu vyote viwili vinategemea nyota chipukizi kama, Desire Doué ambaye naye amekuwa katika fomu bora msimu huu ikiwemo kuisaidia timu hiyo kushinda ubingwa katika fainali ya UCL, huku kwa upande wa, Gonzalo García kutoka ‘academy’ ya Real Madrid Castilla, akitishia kwa kasi ya kufunga mabao.

Shinda mamilioni na Kindege Cha SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini

SEO Banner LV

Majeruhi na watakaokosa mchezo huu

Kwa upande wa PSG

Dembele
Dembele

PSG watacheza bila beki wao chipukizi, Willian Pacho aliyeonyeshwa kadi nyekundu dhidi ya Bayern Munich kwa kumfanyia madhambi Leon Goretzka. Hili linatarajiwa kuwa pigo kubwa kwa PSG kwani mfumo wao wa ‘high press’ unahitaji sana uwezo wake wa kurejesha haraka mpira.

Lucas Hernández pia anatarajia kukosa mechi baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita, Mshambuliaji nyota Ousmane Dembélé amerudi baada ya kupona jeraha la kwapa kiasi cha kuingia akitokea benchi katika mechi mbili zilizopita kama mchezaji wa akiba.

Licha ya majeraha hayo, Dembele alifanikiwa kufunga bao katika mechi ya mwisho dhidi ya Bayern, ambapo alichukua nafasi yake kutoka kwa Bradley Barcola aliyeanza, lakini inatarajiwa Dembélé atarejea kikosi cha kwanza mara baada ya kurejea akiwa katika kiwango bora.

SOMA HII PIA: PSG Vs Arsenal UEFA CL: H2H, Vikosi, uchambuzi, utabiri

Kikosi cha PSG kinachotarajia kuanza

PSG vs Real Madrid Julai 9 2025 live
Kikosi cha PSG

Donnarumma (GK), Hakimi, Marquinhos, Beraldo, Mendes, Neves, Vitinha, F. Ruiz, Doué, Dembélé, Kvaratskhelia.

Mfumo ambao unatarajiwa kutumiwa na PSG ni 4‑3‑3.

Kikosi kamili cha PSG kilicho Marekani ni;

Walinda goli: Gianluigi Donnarumma, Lucas Lavallée, Matvei Safonov, Arnau Tenas.

Wabeki: Lucas Beraldo, Naoufel El Hannach, Achraf Hakimi, Lucas Hernández, Noham Kamara, Presnel Kimpembe, Marquinhos, Nuno Mendes, Willian Pacho, Yoram Zague.

Viungo: Lee Kang‑in, Senny Mayulu, Gabriel Moscardo, João Neves, Fabián Ruiz, Vitinha, Warren Zaire‑Emery.

Washambuliaji: Bradley Barcola, Ousmane Dembélé, Desire Doué, Khvicha Kvaratskhelia, Ibrahim Mbaye, Gonçalo Ramos.

Kuhusu Real Madrid

Kikosi cha Real Madrid
Kikosi cha Real Madrid

Beki chipukizi Dean Huijsen, ambaye amejiunga nao kutokea Bournemouth, anatarajia kutumikia adhabu ya kutocheza mchezo huu mara baada ya mchezo usio wa kiungwana dhidi ya Borussia Dortmund. Raul Asencio au Aurelien Tchouaméni wanaweza kuchukua nafasi yake katika nafasi ya ulinzi.

Kylian Mbappé alianza mashindano haya akiwa na changamoto za tumbo huku nafasi yake ikibebwa na nyota Gonzalo García, ambaye amethibitisha kuwa ‘No Mbappe, no problem’ kwa kufanikiwa kufunga katika kila mchezo wa hatua ya mtoano bila ya Mbappé kuwa sehemu ya kikosi.

Staa wa Brazil, Endrick amejiunga na Real Madrid kwenye Kombe la Dunia la Vilabu na ameanza mazoezi baada ya kupona jeraha la misuli, lakini hakujumuishwa kwenye kikosi cha mzunguko wa 16 bora. Raul Asencio amerudishwa na huenda akawa sehemu ya kikosi cha kocha Xabi Alonso.

Dani Carvajal, Eduardo Camavinga, David Alaba na Ferland Mendy bado hawapo kutokana na majeraha ya muda mrefu.

SOMA HII PIA:Real Madrid vs RB Leipzig: Champions League Clash Preview

Kikosi tarajiwa cha Real Madrid ni;

Courtois (GK), Alexander‑Arnold, Rüdiger, Asensio, F. García, Valverde, Tchouaméni, Bellingham, Güler Vinícius Jr, G. García.

Mfumo unaotarajiwa kutumika ni 4‑4‑2.

Walinda goli: Thibaut Courtois, Fran González, Andriy Lunin, Sergio Mestre.

Wabeki: Diego Aguado, David Alaba, Trent Alexander‑Arnold, Raul Asensio, Dani Carvajal, Jesús Fortea, Fran García, Dean Huijsen, Ferland Mendy, Éder Militao, Jacobo Ramón, Antonio Rüdiger, Lucas Vázquez, Yusi.

Viungo: Jude Bellingham, Eduardo Camavinga, Dani Ceballos, Chema, Arda Güler, Mario Martin, Luka Modrić, Víctor Muñoz, Aurelien Tchouaméni, Federico Valverde.

Washambuliaji: Brahim Díaz, Endrick, Gonzalo García, Kylian Mbappé, Rodrygo, Vinícius Junior.

Hitimisho: Utabiri wa matokeo

Kutokana na kutokuwepo kwa PSG inaweza kupata wakati mgumu wakati wa kupress katikati ya uwanja kupoteza kasi katika press. Kwa upande mwingine, Real Madrid bila Dean Huijsen inatarajia kumtegemea Raul Asencio ambaye ameonyesha kuwa na makosa ya mara kwa mara msimu huu.

Makocha wote wawili ni wa kiwango cha juu na watajaribu kufunika mapungufu hayo, lakini ni ngumu kuyamaliza kabisa, mechi hii inatarajiwa kuwa yenye ushindani mkubwa na mabao mengi, na PSG inaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya ushindi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.