- Yanga SC 2-0 Singida Black Stars, fainali ya kibabe kwenye dakika 90 za jasho funga kazi msimu wa 2024/25.
- Jonathan Sowah wa Singida Black Stars majanga kwenye mchezo wa fainali, alimwa kadi nyekundu.
- Khalid Aucho, Pacome waiongoza Yanga SC kutwaa mataji matano msimu wa 2024/25
Yanga SC 2-0 Singida Black Stars fainali ya kibabe Uwanja wa New Amaan Complex. Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi inafikisha mataji matano msimu wa 2024/25. Ikumbukwe kwamba Juni 25 2025 Yanga SC 2-0 Simba SC, ushindi huo uliwapa taji la Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC.


Magoli ya Yanga SC vs Singida Black Stars
Khalid Aucho alitoa pasi yake ya maelekezo kwa Maxi Nzengeli ambaye alitoa pasi kwa Israel Mwenda. Mwenda akapiga krosi akiwa ndani ya 18 kwa mguu wa kulia na kip awa Singida Black Stars akautema mpira ambao ulikutana na Duke Abuya aliyefunga kwa mguu wa kushoto.
Katika pasi hizo tatu Aucho alitumia mguu wa kushoto, Nzengeli mguu wa kulia. Mwenda alipiga krosi kwa mguu wa kulia na mfungaji alitumia mguu wa kushoto. Yanga SC walitumia dakika 39 kutenganisha ukuta wa Singida Black Stars kwenye fainali iliyokuwa na ushindani mkubwa.
Abuya raia wa Kenya alipachika bao hilo akiwa ndani ya 18 kwa mguu wake wa kushoto. Walinzi zaidi ya wanne ndani ya lango kwa Singida Black Stars walikwama kuokoa hatari hiyo iliyomshinda mlinda mlango.
Jonathan Sowah alipoteza mpira dakika ya 49 kipindi cha pili. Aucho alipoka mpira kwenye miguu ya Sowah kisha Aucho akatoa pasi kwa Nzengeli. Pasi kutoka kwenye miguu ya Nzengeli ilikutana na mshambuliaji Clement Mzize. Mzize alipachika bao la pili dakika ya 49 kwa mguu wa kulia.

Soma hii: Jean Ahoua kubeba tuzo kiatu cha ufungaji bora 2024/25
Mzize ambaye kwenye dakika 45 za mwanzo alikosa nafasi zakufunga, alisubiri mpaka dakika ya 49 kupachika bao la pili na la ushindi kwa Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Singida Black Stars waliyeyusha dakika tatu bila ya uwepo wa nyota wao Sowah. Sowah alionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa kati Ahmed Arajiga. Hii ilitokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano kwenye mchezo huo.
Kikosi cha Yanga SC fainali
Kikosi cha Yanga SC ambacho kilianza dhidi ya Singida Black Stars ni Djigui Diarra, Boka, Israel Mwenda jezi namba 66. Dickson Job ambaye ni nahodha, Bacca, Khalid Aucho, Maxi Nzengeli.
Duke Abuya nyota anayevaa uzi namba 38, Clement Mzize mzawa anayevaa jezi namba 24. Pacome kiungo wa kazi na Mudathir Yahya. Hawa walianza kikosi cha kwanza.
Akiba ni Mshery, Bakari Nondo, Kibwana Shomari. Dennis Nkane. Shekhan, Moses, Farid Mussa. SureBoy, Clatous Chama na Ikangalombo.
Hawa hapa Singida Black Stars
Walioanza kikosi cha kwanza ni Obasogie, Frank Assinki, Ande Koffi, Kennedy Juma, Gadiel Michael. Damaro, Athur Banda, Chuku, Marouf Tchakei. Jonathan Sowah na Keyekeh kwenye fainali dhidi ya mabingwa watetezi Yanga SC.
Mataji matano kwa Yanga SC 2024/25
Yanga SC inakuwa imetwaa mataji matano msimu wa 2024/25 ilianza na Toyota Cup, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara, Kombe la Muungano na CRDB Federation Cup. Taji la funga msimu imetwaa visiwani Zanzibar. Ina kibarua cha kutetea mataji hayo msimu wa 2025/26.
Walitokea hapa Yanga SC

Soma hii: Uongozi wa Yanga SC umeweka wazi vita ya MVP
Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania ilikuwa kete ya Yanga SC kutinga fainali. Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga safari ilianza. Mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwa kiungo wa Yanga SC, Aziz Ki ambaye ni mali ya WydadCasablanca.
Yanga SC imekuwa ikicheza soka la kasi.Safu ya ushambuliaji imekuwa ikifunga mabao mengi jambo lililowapeleka fainali. Kwenye fainali wakiwa ni mabingwa waliwatuliza Singida Black Stars kwa mabao 2-0.
Singida Black Stars waliwaondoa Simba SC
Singida Black Stars ambao ni wageni katika fainali hii, walifanya maajabu katika mchezo wa nusu fainali kwa kuifunga Simba SC mabao 3-1, magoli ya Singida yalifungwa na Jonathan Sowah (17′) na Emmanuel Keyekesh (35′ na 48′)
Kwenye mchezo wa fainali kazi ilikuwa ngumu kwao. Kikombe cha ushindi kikabaki Yanga SC ambao walikuwa ni mabingwa watetezi. Singida Black Stars wamebainisha kuwa ilikuwa ni fainali kubwa na ngumu.
Hussen Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars amesema kuwa watajipanga kwa msimu ujao. Aliongeza kuwa walikuwa wanahitaji taji hilo ila imeshindikana. Licha ya juhudi za wachezaji.
“Ilikuwa ni fainali kubwa na yenye ushindani. Wachezaji wamejituma na mwisho matokeo hayajawa upande wetu. Tutajipanga kwa wakati ujao kufanya vizuri.”


