Yanga vs Simba Juni 15Yanga vs Simba Juni --
  • Yanga SC vs Simba SC inayodhamiriwa Juni 15 2025, Dabi ya Kariakoo ipo, au haipo?
  • Ni itendawili kigumu kama kile cha hadithi ya nani atamfunga paka kengele?
  • Tukio hili lenye ushawishi mkubwa linaangaziwa na zaidi ya nusu ya umma wa mashabiki wa soka ndani na nje ya nchi.
  • Ikumbukwe awali, mchezo huu ulipangwa kufanyika tarehe 8 Machi 2025, lakini uliahirishwa kutokana na mivutano iliyozuka kabla ya pambano hilo.

Maswali ni mengi kuliko majibu Je, Yanga SC vs Simba SC inayodhamiriwa Juni 15 2025, Dabi ya Kariakoo ipo, au haipo? Ni kitendawili kigumu kama kile cha hadithi ya nani atamfunga paka kengele? Ikumbukwe awali mchezo huu ulipaswa kupigwa Machi 8, 2025 kabla ya kuahirishwa kwa sababu zenye utata na kupangiwa ratiba mpya.

Kwanini Yanga SC vs Simba SC inayodhamiriwa Juni 15 2025 Dabi ya Kariakoo ni kitendawili kigumu?

-----------------------------------------------n
Poster ya dabi ya Machi 8

Mchezo wa watani wa jadi kati ya Young Africans S.C. (Yanga SC) dhidi ya Simba SC maarufu kama Derby ya Kariakoo, unatarajiwa kuchezwa tena tarehe 15 Juni 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Ikumbukwe awali mchezo huu ulipangwa kufanyika tarehe 8 Machi 2025, lakini uliahirishwa kutokana na mivutano iliyozuka kabla ya pambano hilo.

SOMA HII PIA: Yanga SC inawadai Simba SC 2024/25

Sababu za kuahirishwa kwa Mchezo Machi 8, ni nini?

Huku maandalizi yote ya mchezo huo yakiendelea kufanyika, ikiwemo ununuzi wa tiketi na mashabiki kujiandaa kuelekea mchezo huo, ghafla Simba SC ilitangaza rasmi kutoshiriki mchezo huo baada ya kudai kuwa ilizuiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Simba SC walileta dai hilo la ukiukwaji wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, zinazoiruhusu timu ngeni kufanya mazoezi kabla ya mechi.

Simba ilidai kuwa wachezaji wake walizuiwa kuingia uwanjani na walinzi wa Yanga SC, jambo lililozua mgogoro mkubwa. Ikumbukwe kwa mujibu wa Kanuni ya 17(45) ya Ligi Kuu, timu ya ugenini ina haki ya kufanya mazoezi uwanjani kabla ya mechi, lakini Simba ilidai kuwa walikosa fursa hiyo kwa sababu ya vizuizi vilivyowekwa na Yanga SC.

 Bodi ya Ligi (TPLB), yaingilia kati

n
Almas Kasongo CEO Bodi ya Ligi

Katika kujibu tuhuma hizo, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa Simba SC ilishindwa kufuata utaratibu sahihi wa kuomba ruhusa ya kufanya mazoezi uwanjani. Hata hivyo, TPLB ilithibitisha kuwa wachezaji wa Simba walizuiwa kuingia uwanjani na walinzi wa Yanga SC, jambo ambalo lilikiuka Kanuni ya 17(45), Kwa hiyo, TPLB iliamua kuahirisha mchezo huo ili kuchunguza.

Yanga wacharuka! Watoa msimamo mzito!

------------------------------------------------n
Hersi Said Rais Yanga

Kufuatia madai hayo uongozi wa Yanga SC, kama timu mwenyeji wa mchezo huo, walikataa kuahirishwa kwa mechi hiyo na walisisitiza kuwa mchezo unapaswa kuchezwa kama ulivyopangwa. Yanga walienda mbali zaidi na kueleza hawatacheza mchezo mwingine badala ya tarehe iliyopangwa awali. Aidha, walidai kuwa TPLB inapaswa kuwapa ushindi kwa mechi hiyo.

Hiyo ikiwa haitoshi Yanga waliweka wazi kuwa hawana imani na baadhi ya watendaji wakuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, na kukomalia kuwa wanahitaji viongozi hao wajiuzulu nyadhifa zao mara moja. Kwa msisitizo mkubwa Yanga wameweka wazi msimamo wa kusema hawatacheza Ng’o mchezo huo, mpaka pale hoja zao zitakapofanyiwa kazi.

SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC, leo ndio leo kwa Mkapa hatoki mtu

Yanga SC yaenda CAS, kesi yao yatupiliwa mbali

Kufuatia mchakato wa shauri lao kuonekana kutoridhiwa na mabosi wa Yanga, waliamua kufungua shauri la kesi kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo CAS, lakini kesi hiyo ilitupiliwa mbali na CAS kwa maelezo kwamba Yanga walishindwa kufuata taratibu za kufungua shauri hilo, kwani walipaswa kuanza na mamlaka za ndani.

Bodi ya ligi yatangaza tarehe mpya ni Juni 15, 2025

Kufuatia majibu hayo ya CAS, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara TPLB ilijiridhisha kupanga upya tarehe ya mchezo huo ambapo walitangaza ngoma hiyo kupigwa Juni 15, mwaka huu. Ambapo katika barua hiyo hawakueleza mustakabali wa mchakato wa uchunguzi ambao ulikuwa ukiendelea kufanyika kuhusu kilichotokea Machi 8, mwaka huu.

Athari za Mgogoro huu kwa Soka la Tanzania

Mgogoro huu umeibua maswali kuhusu usimamizi wa ligi na utekelezaji wa kanuni za soka nchini Tanzania, huku wadau mbalimbali wa soka wakihoji kama TPLB ilifuata taratibu zilizowekwa katika kuahirisha mchezo huo.

Maswali haya yanatoa changamoto kwa viongozi wa soka nchini, kuhakikisha kuwa kuna uwazi na haki katika maamuzi yanayohusu michezo mikubwa kama hii.

Matumaini ya Mchezo wa Juni 15, 2025

Yanga vs Simba Juni --
Yanga vs Simba Juni 15

Ingawa mivutano ya awali ilileta wasiwasi kuhusu ufanikishaji wa mchezo huu, mashabiki wa soka nchini Tanzania wamesalia na kitendawili kujua kama wanatarajia kuona pambano hili la kihistoria likichezwa kwa amani na ufanisi Juni 15? Hasa kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi wa timu hizo mbili kuonekana kukinzana. Simba wanatamba kujiandaa na mchezo huo, huku Yanga wakisema hawachezi.

SOMA HII HAPA: Simba SC ratiba yake Bongo ni bandika bandua, mechi nne siku 10

Utata mwingine kuhusu mchezo huu

Ukiachana na vuta nikuvute hizo, mchezo huu unatarajiwa kuwa na mvuto mkubwa zaidi, hasa kwa kuwa timu zote mbili zinapigania ubingwa wa ligi kuu zikitofautiana kwa pointi moja tu, Yanga wanaongoza msimamo na pointi zao 73, huku Simba wao wakiwa na pointi 72 zikiwa zimesalia mechi mbili kumaliza msimu.

Hitimisho

Derby ya Kariakoo kati ya Yanga SC na Simba SC ni tukio muhimu katika kalenda ya soka la Tanzania. Ingawa mgogoro wa awali ulileta changamoto, matumaini ni kuwa mchezo wa Juni 15, 2025, utaonyeshwa kwa ufanisi na utamaduni wa soka unaokubalika. Mashabiki wanatarajia kuona mchezo wa haki, furaha, na mshindi anayestahili.

Kwa hivyo, tarehe 15 Juni 2025, Uwanja wa Benjamin Mkapa utashuhudia pambano la kihistoria kati ya Yanga SC na Simba SC, ambapo soka la Tanzania litakuwa kwenye macho ya dunia kwa mara nyingine tena katika vita hii ya kihistoria.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.