DiarraDiarra
  • Moussa Camara wa Simba SC anaongoza chati ya vinara wa kuwa na hati safi nyingi kwenye ligi kuu bara.
  • Djigui Diarra wa Yanga SC kwenye chati naye aiangia kwenye orodha ya wale wanaowania tuzo ya kipa bora.
  • JKT Tanzania kipa wakuokoa michomo mpaka akaitwa timu ya taifa ya Tanzania.

Tuzo ya kipa bora 2024/25 Camara wa Simba SC na Diarra wa Yanga SC vitani kuwania tuzo hiyo kutokana na kazi yao wanayoifanya ndani ya uwanja katika kutimiza majukumu yao.

Vita kubwa ni makipa kutoka mtaa wa Kariakoo, Simba SC na Yanga SC ambao hawa wanavutana mashati kwa asilimia kubwa katika kuwania tuzo hiyo.

Soma na hii: Camara kwenye vita na Diarra, ratiba hii hapa – SportPesa Tanzania

Hapa tunakuletea orodha ya makipa wanaowania tuzo ya kipa bora na rekodi zao namna hii:-

Moussa Camara wa Simba SC

M- Camara
Moussa Camara, kipa namba moja wa Simba SC. Source: Simba SC.

Kipa namba moja wa Simba SC ana hati safi kibindoni 17. Kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Singida Black Stars uliochezwa Uwanja wa KMC Complex alifikisha hati ya 17.

Katika mchezo huo uliochezwa Mei 28 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 1-0 Singida Black Stars. Bao la ushindi lilifungwa na Steven Mukwala.

Simba SC kwenye msimamo ni nafasi ya pili ikiwa na pointi 72 baada ya kucheza mechi 27. Ni mabao 11 Camara amefungwa ndani ya ligi akikaa langoni kwenye mechi 25.

Safu ya ushambuliaji ya Simba SC imefunga jumla ya mabao 63 ikiwa ni timu namba mbili kufunga mabao mengi ndani ya ligi.

 Djigui Diarra wa Yanga SC

Diara
Diara kipa namba moja wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Kipa namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra yeye ni namba mbili kwenye kukusanya hati safi. Akiwa nazo hati 15 ndani ya ligi msimu wa 2024/25.

Yanga SC ni namba moja kwenye ligi ikiwa na pointi 73 kibindoni baada ya kucheza mechi 27. Safu ya ushambuliaji ya Yanga SC imefunga mabao 71.

Ni mabao 10 ukuta wa Yanga SC umeruhusu ikiwa ni timu namba moja kufungwa mabao machache.

Diarra amekuwa ni mshindani mkubwa wa kipa namba moja wa Simba SC, Moussa Camara kwenye kuwania tuzo ya kipa bora.

 Patrick Munthary wa Mashujaa

Patrick Munthary wa Mashujaa FC naye anaingia kwenye orodha ya mashujaa wakiwa langoni. Ana hati safi 12 kwa msimu wa 2024/25.

Mashujaa FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 8 ni uhakika kushiriki ligi msimu ujao kwa kuwa haitashuka daraja.

Safu ya ushambuliaji ya Mashujaa FC ni mabao 28 imefunga huku ukuta ukiwa umeruhusu mabao 32.

Pointi zao walizonazo kibindoni Mashujaa FC ni 33 baada ya mechi 28 ndani ya ligi.

 Mohamed Mustafa wa Azam FC

Matajiri wa Dar, Azam FC kipa wao hajakosekana kwenye wakali wakukusanya hati safi ndani ya ligi.

Ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 57 baada ya mechi 28. Mabao yakufungwa ni 17. Kipa Mustafa amekusanya hati safi 10.

Azam FC safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 48 ikiwa ni timu namba tatu kufunga mabao mengi.

Yona Amosi wa Pamba Jiji

Pamba Jiji sio wepesi kwenye eneo la mlinda mlango kwani wanaye kipa mwenye uwezo wa kuokoa hatari nyingi. Ni Yona Amosi mwenye hati safi 10.

Kwenye msimamo Pamba Jiji ya Mwanza ipo nafasi ya 12 imekusanya pointi 30 baada yakucheza mechi 28.

Safu ya ushambuliaji ya Pamba Jiji imefunga jumla ya mabao 20 na ukuta umeruhusu mabao 32.

Yakoub Suleman wa JKT Tanzania

Yakub
Yakub kipa namba moja wa JKT Tanzania. Source:JKT Tanzania.

Yakoub wa JKT Tanzania ana hati safi 8. Uwezo wake wa kuoka hatari akiwa langoni ulima nafasi kuitwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania.

JKT Tanzania kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 35 kibindoni. Safu ya ushambuliaji imefunga mabao 27 na ukuta umeruhusu mabao 26.

 Ngeleka Katembua wa Dodoma Jiji

Watoto wa makao makuu, Dodoma Jiji ni nafasi ya 7 kwenye msimamo wapo kwa sasa baada ya mechi 28.

Kipa Ngeleka yeye ana hati safi 7 ndani ya ligi msimu wa 2024/25 akiwa ni miongoni mwa makipa waliokusanya hati safi nyingi.

Dodoma Jiji safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 30 na kuruhusu mabao 42 na pointi zao ni 34.

 Metacha Mnata wa Singida Black Stars

Alianza Metacha Mnata kuwa kipa namba moja wa Singida Black Stars, ila ghafla namba ameanza kuipoteza.

Ni hati safi 7 anazo kibindoni ndani ya ligi. Singida Black Stars kwenye msimamo ni nafasi ya nne baada ya mechi 28.

Safu ya ushambuliaji imefunga mabao 40 na ukuta umeruhusu mabao 22. Pointi zao ni 53 kibindoni.

Tuzo ya kipa bora itapatikana mwisho wa msimu na kipa mwenye hati safi nyingi atakabidhiwa tuzo hiyo iliyokuwa mikononi mwa Ley Matampi wa Coastal Union.

Share this: