KUMEANZA kuchangamka ndani ya Yanga kuelekea kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Hilal ya Sudan ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa Novemba 26 2024 Uwanja wa Mkapa kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu ndani ya dakika 90.
Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ipo hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kete yake ya kwanza itakuwa ugenini huku uongozi ukiweka wazi kuwa una kisasi cha kuwalipa wapinzani hao kimataifa ndani ya dakika 180 kwa kusaka ushindi nje ndani.

Timu mbili kutoka Tanzania zinapeperusha bendera kimataifa ambapo kwa upande wa Simba ni Kombe la Shirikisho Afrika hawa watakuwa na kibarua Novemba 27, Uwanja wa Mkapa itakuwa dhidi ya Bravos ya Angola.
Mechi ya Yanga imepewa jina la Dube Day nyota ambaye ni mshambuliaji, ingizo hili jipya kwenye mechi za ligi msimu wa 2024/25 hajafunga bao licha ya kupata nafasi katika mechi hizo zama zile za Migue Gamondi ambaye amekutana na mkono wa asante.
Tayari Yanga imezindua jezi mpya kwa ajili ya mashindano hayo ya kimataifa ambazo zipo sokoni sasa wote walinzindua siku moja na mtani Simba ilikuwa ni Novemba 20 2024.
MATIZI BALAA ZITO
Prince Dube ni miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye mazezi ya mwisho kuelekea mchezo huo huku wakipewa matizi ya maana yatakayowapa matokeo mazuri kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbali na Dube, Clatous Chama kiungo mshambuliaji, Jean Baleke ambaye ni mshambuliaji, Aboutwalib Mshery na Djigui Diarra haw ani makipa nao wapo kwenye orodha ya nyota wa Yanga wanaoendelea na mazoezi.
SEMAJI TAMBO KIMATAIFA

“Jumanne ni siku ambayo Tanzania yote itatulia na kuufatilia mchezo wetu dhidi ya Al Hilal, kocha wetu ‘German Machine’ Sead Ramovic ametambulisha soka linaloitwa ‘GUSA ACHIA TWENDE KWAO’ baada ya kutazama hili soka mazoezini nikaona kabisa Wananchi tunakwenda kupata raha siku ya Jumanne.
“Niwaombe msiwe watu wa kuikosa furaha hii, tukate tiketi muda huu tukutane Benjamin Mkapa kufurahi. “Tunafahamu kuwa mchezo wetu dhidi ya Al Hilal utakuwa mgumu lakini kwa umoja wetu, kwa wingi wetu, kwa hamasa tutakayowapa wachezaji wetu, mchezo huu utakuwa mwepesi na tutashinda.
“Wachezaji wetu wapo tayari, Bechi la Ufundi lipo tayari na viongozi wetu wapo tayari, kazi iliyobaki ni kwetu sisi Wananchi, jukumu letu ni kuwasapoti wachezaji wetu, basi tukate tiketi kwa wingi na twende kwa wingi kuishangilia Yanga.
“Siku ya mchezo natamani kumuona kila Mwananchi akiwa uwanjani kuwapa hamasa wachezaji wetu. Safari hii tumepata mwalimu anayependa shangwe la mashabiki.Yeye anatamani kuwaona siku hiyo mashabiki. Niwaombe tu Wananchi Wenzangu, tukate tiketi mapema tusisubiri siku ya mechi ifike hapo tuanze kuwa kwenye mahangaiko hapana tuanze maandalizi mapema.
“Safari hii hatutamani kabisa zile hesabu za kuomba fulani afungwe ili tufuzu, mnakumbuka msimu uliopita hatukuanza vizuri mechi yetu ya kwanza kule Algeria. Niwambie Wanayanga wote safari hii tunapaswa kuchukua pointi 3 kwenye mechi zote za nyumbani, hivyo basi tunawahitaji sana uwanjani siku hiyo.
“Sisi tunamtazama kwa sasa Al Hilal kwa jicho la roho mbaya tu. Hatuna msalie mtume siku ya Jumanne, hatukumalizana naye vizuri kwahiyo tuna kisasi naye na mechi zetu mbili za mwisho za ligi ndiyo zinampa wakati mgumu Al Hilal.
HUYU HAPA MZEE WA GUSA ACHIA

Kocha mpya wa Yanga, Sead Ramovic ambaye ametambulisha aina mpya ya soka inayokwenda kwa jina la gusa achia ameweka wazi kuwa wanatambua watakuwa na kazi ngumu kwenye mchezo wao wa kimataifa kwa kuwa bado hajaunda kikosi kazi vizuri.
“Unajua mimi nipo hapa na siku ambazo nimeanza nazo huwezi kusema ni nyingi kwani hata ukiwa unakwenda kufanya mazoezi ya kujenga mwili hautafanikiwa kubadilika ndani ya siku sita, ipo wazi unahitaji muda kuwa bora.
“Kwa namna ambavyo tumeanza hatupo vibaya nina amini tunakwenda kufanya vizuri na tutazidi kuimarika kadri ambavyo siku zinakwenda, wachezaji wapo vizuri na wanapenda kuona timu inapata matokeo tuna amini kwamba tutapambana ili kuwa imara kwenye mechi zetu zote.”

